Latest Post
Showing posts with label MAGAZETI. Show all posts
Showing posts with label MAGAZETI. Show all posts
00:34
PICHA:SHOW YA DIAMOND KWENYE UFUNGUZI WA MSASANI CITY MALL
Written By Unknown on Saturday, July 6, 2013 | 00:34
00:28
Timu
kubwa na yenye nguvu sana kwenye soka la Croatia haikufanya vizuri
katika hatua ya makundi ya michuano miwili iliyopita ya Champions
League. Kati ya michezo 12 waliyocheza, walipata pointi moja tu kati ya
36. Hwakufanya vizuri kabisa kwenye michuano hii, lakini kwao kucheza tu
ilitosha sana. Lakini Dinamo Zagreb imetoa vipaji vingi sana kwenye
soka na tunavifurahia vipaji hivyo shukrani kwa mtu mmoja aitwaye
Zdravko Mamic.
ZDRAVKO MAMIC: 'JORGE MENDES' WA CROATIA ANAYEKULA ASILIMIA 20 YA MSHAHARA YA LUKA MODRIC - AGEUZA DINAMO ZAGREB KIBONDE KWA KUIPA UTAJIRI
Zdravko
Mamic ni ni mkurugenzi wa michezo wa Dinamo. Amekuwa maarufu sana kwa
tabia yake ya kuwatolea maneno machafu baadhi ya waandishi wa habari,
akiwatishia kuwafanyia vurugu na kuwatukana wao na kazi yao. Pia amekuwa
akihusishwa sana na sajili tata za wachezaji hasa wa nchi hiyo. Aliwahi
kukamatwa baada ya kumtukana waziri wa michezo wa Croatia, lakini
pamoja na vituko kocha huyu ana mazuri yake. Ni genius linapokuja suala
la kufanya biashara ya wachezaji.
Katika
kipindi cha miaka 10, tangu Zdravko Mamic ajiunge na Dinamo Zagreb,
klabu hiyo imejipatia kiasi cha 160 million kutokana na mauzo ya
wachezaji.
Dinamo
Zagreb sio timu inayofanya biashara ya kuuza sana wachezaji barani ulaya
kama ilivyo kwa Porto, lakini hawapo mbali kwenye. Benfica na Udinese
pia nao wanafuatia, lakini inabidi vilabu hivi vyote vina misuli ya
kifedha kuliko klabu hii ya Croatia.
![]() |
| Luka Modric mmoja ya wachezaji wanamuingizia fedha nyingi Mamic |
Mamic
anapata fedha nyingi kwa kukubali kuwauza wachezaji kwenda kwenye vilabu
vikubwa. Mfano mzuri ni dili aliloingia na Luka Modric - walikubaliana
na mchezaji huyo kupata asilimia 20 ya mshahara wake atakaokuwa akilipwa
na klabu yake. Pia dili hilo limeendelea mpaka sasa mchezaji huyo akiwa
na Real Madrid - kwa makataba wa miaka mitano na Madrid - Luka Modric
atampatia kiasi kisichopungua 900 000 Euros Zdravko Mamic.
Tangu awe mkurugenzi wa ufundi wa Dinamo mwaka 2003, ameshawabadilisha makocha 15 tofauti - waliokuwa wanatofautiana nae kwenye suala la kuuza wachezaji pale anapoona kuna maslahi yake yake binafsi.
BAADHI YA UHAMISHO WALIOWAHI KUFANYA DINAMO ZEGREB
Luka Modric to Tottenham , €21 million
Mateo Kovacic to Inter Milan , €15 million
Eduardo da Silva to Arsenal, , €15 million
Vedran Corluka to Manchester City, , €13 million
Dejan Lovren to Lion , €9.5 million
Mario Mandzukic to Wolfsburg, , €9 million
Pia hivi sasa Mamic yupo katika mazungumzo na Tottenham katika kukamilisha baishara ya kuwauza wachezaji wawili Tin Jedvaj na Alen Halilovic ambaye anatajwa kuwa mrithi wa Luka Modric. Dili hilo linatajwa kuwa na thamani ya zaidi ya paundi millioni 18 - na hapo Mamic ana kato lake pamoja na kuwa na mikataba binafsi na wachezaji hao wawili.
Taarifa nchini Croatia zinasema Mamic yupo katika matayarisho ya kuanzisha kampuni ya uwakala wa wachezaji, ili kufuata nyayo za wakala maarufu barani ulaya Jorge Mendes.
Taarifa nchini Croatia zinasema Mamic yupo katika matayarisho ya kuanzisha kampuni ya uwakala wa wachezaji, ili kufuata nyayo za wakala maarufu barani ulaya Jorge Mendes.
00:27
PICHA YA SIKU: BARCELONA WAMUONDOA THIAGO ALCANTARA KWENYE TANGAZO LA JEZI NA TOUR KWENYE AKAUNTI YAO YA INSTAGRAM
![]() |
| Picha ya juu inaonyesha ilivyokuwa mwanzo Thiago akiwepo - wakati hii ya chini ni ya leo ikiwa sura ya Thiago Alcantara haijakwatwa. |
00:26
West Brom wamethibitisha kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Ufaransa Nicolas Anelka.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 34, ambaye alikuwa huru, amesaini mkataba wa kuanzia wa mwaka mmoja wa kuichezea klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya England.
Klabu hiyo imethibitisha kupitia akaunti yake ya Twitter: 'Albion leo usiku imekamilisha usajili wa @anelkaofficiel kwa mkataba wa mwaka mmoja, huku kukiwa na hivyo.'
Kocha wa Baggies Steve Clarke, ambaye alishafanya kazi na Anelka kwa muda mfupi ndani ya klabu ya Anelka amefurahia usajili huo.
'Tulikuwa tunakosa nguvu ya ziada kwenye ushambuliaji kutoka mwaka jana, tunajaribu kuweka hilo sawa - na kwa kuanzia kwa usajili wa Nicolas,' aliuambia mtandklabu hiyo wba.co.uk.
Anelka sasa anazidi kujiandikia rekodi ya kuwa mchezaji aliyevicheza vilabu vingi kwenye ligi kuu ya England baada ya kuitumikia Arsena, Chelsea, Liverpool, Manchester City, Bolton
NICOLAS ANELKA ARUDI TENA ENGLAND - ASAJILIWA NA WEST BROM NA KUWEKA REKODI YA KUCHEZEA KLABU 6 ZA LIGI KUU YA ENGLAND
West Brom wamethibitisha kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Ufaransa Nicolas Anelka.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 34, ambaye alikuwa huru, amesaini mkataba wa kuanzia wa mwaka mmoja wa kuichezea klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya England.
Klabu hiyo imethibitisha kupitia akaunti yake ya Twitter: 'Albion leo usiku imekamilisha usajili wa @anelkaofficiel kwa mkataba wa mwaka mmoja, huku kukiwa na hivyo.'
Kocha wa Baggies Steve Clarke, ambaye alishafanya kazi na Anelka kwa muda mfupi ndani ya klabu ya Anelka amefurahia usajili huo.
'Tulikuwa tunakosa nguvu ya ziada kwenye ushambuliaji kutoka mwaka jana, tunajaribu kuweka hilo sawa - na kwa kuanzia kwa usajili wa Nicolas,' aliuambia mtandklabu hiyo wba.co.uk.
Anelka sasa anazidi kujiandikia rekodi ya kuwa mchezaji aliyevicheza vilabu vingi kwenye ligi kuu ya England baada ya kuitumikia Arsena, Chelsea, Liverpool, Manchester City, Bolton
VILABU VYOTE ALIVYOCHEZEA ANELKA
| Senior career* | |||
|---|---|---|---|
| Years | Team | Apps† | (Gls)† |
| 1996–1997 | Paris Saint-Germain | 10 | (1) |
| 1997–1999 | Arsenal | 65 | (23) |
| 1999–2000 | Real Madrid | 19 | (2) |
| 2000–2002 | Paris Saint-Germain | 39 | (10) |
| 2001–2002 | → Liverpool (loan) | 20 | (4) |
| 2002–2005 | Manchester City | 89 | (37) |
| 2005–2006 | Fenerbahçe | 39 | (14) |
| 2006–2008 | Bolton Wanderers | 53 | (21) |
| 2008–2012 | Chelsea | 125 | (38) |
| 2012–2013 | Shanghai Shenhua | 22 | (3) |
| 2013 | → Juventus (loan) | 3 | (0) |
| 2013– | West Bromwich Albion | 0 | (0 |
00:24
Cameroon imefungiwa kwa muda na FIFA kufuatia serikali ya nchi hiyo kujiingiza katika masuala ya chama cha soka nchini humo.
Tangazo la FIFA limesema kwamba kamati ya dharura ya shirikisho hilo la soka duniani imeamua kusimamisha kwa muda chama cha soka cha Cameroon FECAFOOT na uamuzi huo umeanza kutekelezwa mara moja kwa sababu serikali inaingilia masuala ya chama cha soka
Taarifa hizi zimekuja saa moja baada ya Cameroon kuzawadiwa pointi 3, kuwarudisha kwenye uongozi wa kundi I, baada ya Togo kuadhibiwa kwa kumchezesha mchezaji Jacques Alexys Romao, ambaye hakupaswa kucheza wa mwezi uliopita baina ya timu hizo mbili.
Hatua hii ya FIFA inawazuia Indomitable Lions kucheza mchezo wao muhimu wa kufuzu dhidi ya Libya September 6.
Taarifa rasmi ya FIFA ilisema: “"kamati ya dharula ya FIFA imeamua kufungia chama cha soka cha soka cha Cameroon kutokana na serikali ya nchi hiyo kuingilia masuala ya soka ya chama hicho.
“Wakati wa kipindi cha kifungo hichi, Fecafoot inaweza isiwakilishwe katika michuano yoyote ya inayosimamiwa na FIFA na CAF, kuanzia ngazi ya taifa kwenye vilabu kwenye mechi za mashindano mpaka kirafiki."
CAMEROON YAFUNGIWA NA FIFA BAADA SERIKALI KUINGILIA MASUALA YA SOKA