Latest Post
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts

PICHA ZA SIKU: MASHINDANO YA MAGARI YA GHARAMA YASIYO RASMI YA WACHEZAJI WA MAN UNITED: ANDERSON KIBOKO AINGIA MAZOEZINI NA GARI LA MILLION 286

Written By Unknown on Saturday, July 6, 2013 | 00:21


MERC-URIAL TALENT ... Anderson turns up in his £168,395 SLS    Anderson akiingia na gari yake aina ya Mercedez yenye thamani ya  £168,395 
 
Leo asubuhi wachezaji wa Manchester United walikuwa na mashindano yasiyo rasmi ya kuonyesha magari yao ya thamani wakati wakiwasili kwenye uwanja wao wa mazoezi AON Carrington. Mchezaji wa kibrazil Anderson pamoja na kutokuwa mmoja ya wachezaji wanaolipwa fedha nyingi sana na United - yeye ndio alikuwa mchezaji aliyekuja na gari la thamani zaidi Mercedez ambalo linauzwa kiasi cha millioni 286,271,500 za kitanzania.
 

Rio Ferdinand — Jaguar XJ Portfolio (£70,385)

Rio Ferdinand

Wayne Rooney — Range Rover Sport Autobiography (£84,895)

Rooney

Nemanja Vidic — Mercedes M Class (£47,385)

Vidic


Ryan Giggs — Range Rover Sport Autobiography (£98,395)

Giggs

Phil Neville — Porsche Cayenne (£86,895)

Neville

Rafael and Fabio da Silva — Chevrolet Captiva (£32,000)

Fabio & Rafael

Michael Carrick — Mercedes M Class (£47,386)

Carrick

Ashley Young — Range Rover Sport Autobiography (£68,995)

Young

Alex Buttner — Chevrolet Camaro Coupe (36,785)

Buttner

BREAKING NEWS: MOYES ASEMA: ROONEY HAUZWI, ATAENDELEA KUWA MCHEZA WA UNITED - KUHUSU RONALDO ASHINDWA KUKATAA WALA KUKUBALI KUTAKA KUMSAJILI


Kocha wa Manchester United David Moyes leo hii amethibitisha kwamba mshambuliaji wa klabu hiyo Wayne Rooney hayupo sokoni na ataendelea kuicheza klabu hiyo kwa mingi ijayo.

Akizungumza kwenye mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu ajiunge na klabu hiyo akichukua nafasi ya Sir Alex Ferguson, Moyes alisema: "Nimeongea na Wayne Rooney. Wayne yupo nyuma ya mabao 40 kumfikia Sir Bobby na Denis Law. Wayne hauzwi - ni mchezaji wa Manchester United - na ataendelea kubakia kuwa mchezaji wa Manchester United. Nimekuwa na mikutano nae kadhaa. Amerudi kwenye hali nzuri na anafanya vizuri mazoezini. Tunajaribu kufanya kila kitu kumrudisha Wayne Rooney kuwa kama alivyokuwa zamani - Wayne Rooney ambaye tunamjua.

"Vyovyote vilivyotokea kabla, tunafanya kazi pamoja sasa. Macho yake yanaonyesha ni mtu mwenye furaha, ni lazima niseme Wayne hauzwi. Kuliwahi kuwepo mkutano wa siri baina ya Rooney na Sir Alex. Mie naendelea mbele sasa, sijui nini kilizungumzwa kwenye mkutano huo. Ninachofikiria sasa ni kusonga mbele na kufanya kazi ya kumrudisha Wayne Rooney kwenye ubora wake. "


Alipoulizwa kuhusu Cristiano Ronaldo, Moyes alijibu: "Sitomzungumzia yeye moja kwa moja na wachezaji wengine wa vilabu vingine. Lakini hii klabu siku zote imekuwa ikivutiwa na wachezaji bora duniani."

Pia Moyes alithibitisha kwamba winga mpya wa klabu hiyo aliyesajiliwa kutoka Crystal Palace - Wilfred Zaha ambaye amekuwa akiwindwa na vilabu vingi kujiunga navyo kwa mkopo - Moyes amesema mchezaji huyo ataungana na Manchester United kwenye tour ya pre-season, kama ilivyo kwa wachezaji wengine. 

Wakati huo huo alipoulizwa kuhusu usajili wa wachezaji wapya, Moyes amesema angependa kusajili wachezaji mapema lakini mambo yamekuwa yakichelewa kutokana na makocha ambao ndio wanaothibitisha uuzwaji wa wachezaji wengi wamekuwa likizo au ndio wanaingia kwenye vilabu vyao vipya.

KALI YA LEO: DORTMUND WATAMBULISHA JEZI YAO MPYA KWA KUTUMIA MAUA YALIYOPANDWA KWENYE BUSTANI


Borussia Dortmund wamezindua jezi yao mpya ya nyumbani watakaovaa msimu ujao na wamefanya hivyo kwa namna ya kipekee. Watengenezaji wa jezi zao Puma walitengeneza mfano wa jezi za nyumbani za Borussia kwa kutumia maua yasiyopungua 80,600 kutengeneza mfano wa jezi katika bustani ya Dortumund Westfalenpark. 
Kutoka BVB.de:
Usiku wa alhamisi, PUMA ilipanda maua 80,645 , ambayo ni idadi sawa ni ya washabiki wanaoweza kuingia kwenye uwanja wa Dortmund  SIGNAL IDUNA PARK, walifanya hivi katika kubuni na kutambulisha jezi mpya - kwa kutumia maua tofauti ya njano na rangi nyeusi. 

NEYMAR KIBOKO: ASILIMIA 20 YA WATOTO WANAOZALIWA BOLIVIA HIVI KARIBUNI WAPEWA JINA LAKE



Mchezaji wa bora wa mashindano ya kombe la mabara  Neymar ana miaka 21 tu , lakini ni mmoja ya wachezaji wa Amerika ya Kusini ambao wanaweza kuwafanya watu wazimie kwa kujawa na furaha kwa kumuangalia tu mchezaji huyo wa kibrazili na huku akiwa anakaribia kujiunga rasmi na Barcelona, umaarufu wake unaweza ukazidi kukua mpaka kwenye mabara mengine. 
Katika kuonyesha ni namna gani anakubalika huko barani Amerika, watu nchini Bolivia wamewapa watoto wao jina la Neymar katika hali ya kumtukuza winga huyo wa kibrazili. 
Kutoka Sambafoot:
Kwa mujibu wa gazeti la Bolivia La Razon, watoto wawili kati y 10 wanaozaliwa kwenye nchi hiyo wamekuwa wakipewa jina la mchezaji huyo wa selecao. Na wanatabiri kwamba suala hili litazidi kukua kwa kuwa hata baadhi ya wanaume hasa kwenye mji wa La Paz wamekuwa wakijipa jina la nyota huyo wa Barcelona
           "Tunaamini miaka 17 ijayo vijana wengi wa wakati huo watakuwa na jina la Neymar kwa sababu ya huu mtindo mpya ulioingia,' alisema msajili wa raia Remigio Condori .

DENT WA MWAKA WA KWANZA AIBA SIMU AINA YA BLACKBERRY NA KUIFICHA SEHEMU ZA SIRI:BALAA LAKE SASA SHUHUDIA MWENYEWE

Tukio hili limetokea huko Nigeria ambapo binti anayesemekana ni wa mwaka wa kwanza alikwenda kutembea katika hostel za wenzake na alipopata mwanya akaiba simu aina ya Black Berry. Hata hivyo baada ya mwenye simu kushtuka binti huyo aligoma kuichukua simu hiyo na ndipo watu walipoamua kuipiga simu na kuanza kuita ikiwa sehemu za siri. Baada ya tukio hilo wavulana kutoka vyumba vya pembeni walikuja na kumsachi huku wakimvua nguo, hakuwa na la ziada zaidi ya kuwa mpole wakati watu wakimpiga picha hizo za aibu
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. harod tz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger