Latest Post

ngekuwa wewe Ungefanyaje ?? Balaa Hili

Written By Unknown on Saturday, July 6, 2013 | 01:27

Mdada mmoja mke wa mtu alikuwa akisumbuliwa sana na jamaa mmoja aliyekuwa akimtaka kila siku, hatimae akamwambia mumewe. Mume akamwambia mkewe, we kubali tuu, ila mwambie aje mlale hapa kwetu, mi ntajificha uvunguni na panga. Akisha ingia ukiona kamaliza kuvua nguo we ning’iniza mkono anza kuuchezesha, mi nikiuona ntatoka uvunguni na kumfunza adabu. Mdada akafuata masharti ya mumewe na hatimae wakaingia chumbani na yule bwana , mumewe akiwa tayari na panga uvunguni mwa kitanda. Jamaa alipovua shati, mke alishangaa kuona ana makovu makubwa kifuani na mgongoni; MKE: Heee mbona una makovu hivyo?? JAMAA: Niwe mkweli tuu, kwako dia!! mie nina tatizo sana la kupenda wake za watu, waume wengi wamekuwa wakipanga kunifumania, nilishafumaniwa mara kumi na tisa, na wote walionifumania niliwaua. Ila jaribio la mwisho nilidakwa na mapolisi nikatumikia kifungo cha miaka 27 jela, Lakini ninavyopenda wake za watu sitaacha kuua. Hivi sina muda tangu nitoke huko jela hivyo nina ukame wa punda na nilipokuona moyo wangu ukakudondokea. Na nitatulia na wewe. MKE: Heee! Haiwezekani jamani!!….jamaa akaendelea kuvua nguo alipomaliza mdada akaanza kujitahidi kuning’iniza mkono ili mumewe atoke uvunguni aje kumuokoa, mume akabana kimya, kila mdada akijitihadi kupunga mkono hakupata jibu, mdada akalalamika mpaka jamaa akamaliza shughuli zake akatokomea. MKE: Huku akilia, ndio nini umenifanyia? Mbona hukutoka?? MUME: We we we, Weeeee mama naniii!!.. mwenyewe umesikia keshaua 19 ulitaka niwe wa ishirini?

PASTOR NA MAHUBIRI MARA MAMA MMOJA KAANZA KULIA.

Pastor mmoja alikuwa akihubiri kanisani, mara akamuona
mama mmoja akilia kwa uchungu sana.
Pastor akajua yule  mama amechomwa na mahubiriyake, akazidi kuongeza dozi yamaneno.
Baada ya mahubiri pastor akamuita yule mama na kumuuliza nini kinacho kuhuzunisha.
Huku akiendelea kulia akasema,"Yaani mchungaji kilanikiona hizo ndevu zako namkumbuka mbuzi wangu beberu aliyeibiwa...na pata uchungu mno mpaka naishia kulia."

HAYA NDIO MAPENZI YA SIKU HIZI. DUUH !!


JAMAA:"I love you swty."
DEM:"I love you too...ila tupendane tu,mambo ya ngono sitaki namtunzia mume atakaenioa."
JAMAA:"Hilo si tatizo,na mimi mambo ya kuniomba pesa sitaki namtunzia mke nitakaemuoa!"

CHEKA NA WEWE

TOTO:"Sababu sina akili."
BABA:"Ooh,sasa ngoja nikupige fimbo za kutosha ili
uwe na akili mshenzi
wewe!"
MTOTO:"Ingekuwa fimbo ndio
humfunza mtu kuwa na akili,basi punda
na farasi wangekuwa MAPROFESA."





2. Watoto wawili walirudi kwao na
majibu ya mtihani wa mwisho wa
muhula;
BABA:"Safi sana naona umepata
A katika masomo yako yote." Diana unataka zawadi gani?
DIANA:"Nataka kwenda kusoma AUSTRALIA."
BABA:"Na wewe Tina naona
umepata E masomo yote! Ndo
nini hii?"
TINA:"Nataka kwenda kusoma
England!"






Usafi tuliomuonyesha Obama udumishwe


Kwa takribani wiki moja iliyopita wakazi wa jiji la Dar es Salaam walishuhudia mji wao ukiwa msafi kama ambavyo uliwahi kuwa huko nyuma kati ya mwaka 1996-2000 halmashauri ya ya Jiji la Dar es Salaam ilipovunjwa baada ya kushindwa kukidhi vigezo vyote vya uwajibikaji hasa eneo la usafi, na badala yake ikaundwa Tume ya Jiji iliyoongozwa na Mwenyekiti wake, Charles Keenja.

Usafi huu ulishuhudiwa kila kona, hasa kwenye barabara kuu na mitaa ya katikati ya Jiji. Tumeshuhudia msako mkali wa wachuuzi maarufu kama wamachinga; tumeona mama lishe na baba lishe nao wakifurushwa sehemu mbalimbali ambazo kimsingi siyo za kufanya biashara.

Operesheni hii ilikuwa nzito. Polisi waliobeba silaha walikuwa nyuma ya askari mgambo waliokuwa wanapita kila mtaa wakivunja meza za wachuuzi, wakivunja vibanda vyao na kuondoka na bidhaa zilizokuwa zinauzwa; kuna maeneo baadhi ya wachuuzi walikamatwa.

Ilikuwa ni wiki ya mikikimikiki ili kufanikisha kazi ya kuliweka Jiji hilo katika hali ya usafi ili ugeni mkubwa wa Rais Barack Obama, amabo uliingia nchini juzi na kuondoka jana, usikutane na hali ya kutufedhehesha, uchafu. Uchafu ni aibu, siyo sifa njema.

Kwa kujua ukweli huo kwamba uchuuzi wa ovyo ovyo kila mahali, kila kona unachangia kuchafua Jiji, na kwa kuelewa kwamba kote walikotanda wachuuzi waliofurushwa hawaruhusiwi kisheria, basi manispaa zote za Dar es Salaam, kuanzia Temeke, Ilala hadi Kinondoni zikaendesha operesheni kabambe ya kusafisha maeneo yao.

Tunashukuru kwamba operesheni hii walau umetusetiri na aibu mbele ya ugeni huu mkubwa ambao umetujengea jina zuri kimataifa kwamba Tanzania ipo na inavuma. Ziara ya Obama imeacha mengi, lakini kubwa ambalo halina ubishi ni ukweli kwamba imeitangaza Tanzania kila kona ya dunia hii. Ni bango kubwa la kibiashara, la kuvutia wawekezaji, la kuweka wazi kwamba tupo na tunakubalika kimataifa.

Kwa hiyo, wenye mamlaka katika manispaa hizi tatu wamejua vilivyo kwamba walikuwa na wajibu wa kutimiza wajibu wao walau kwa muda wa wiki moja tu ili maeneo yetu yawe safi; kwamba ilifika mahali siyo tu barabara ambazo tumezoea kuona kina mama waliochoka wakifagia kwa kutumia zana duni mno, yalipatikana magari ya kufagia, yalipatikana magari ya kumwaga maji barabarani, lakini pia yalipatikana ya kusugua lami (kudeki) ili ing’ae isituaibishe.

Viongozi wetu wanasafiri sana nje. Wakifika kwenye miji ya wenzetu huko nje, wanajionea wenyewe kwanza ilivyopangwa, pili ilivyo safi. Usafi ni mojawapo ya sifa muhimu kwa kila mji, wanaochaguliwa kwenye miji hii wakiomba kura kwa wananchi wao pamoja na mambo mengine wanayoahidi ni kuendeleza sifa njema ya kuwa na mazingira bora ya kuishi. 

Yaani kuhakikisha taka ngumu na za vimiminika zinaondolewa kwenye makazi ya watu, kuhakikisha kwamba barabara bora zaidi zinajengwa na zilizopo zinatunzwa, lakini la umuhimu zaidi kuwahakikishia wakazi wa miji hiyo usalama wa afya zao wakati wote.

Tanzania siyo kisiwa, miji yake yote ukiwamo Dar es Salaam unapashwa kuwa msafi, ivutie wageni, ivutie na kuwapa amani wakazi wake, ipangwe ili kuepuka kero mbalimbali za misongamano isiyokuwa ya lazima; kwa bahati mbaya kinyume chake ndiyo uweli wa mambo. Ukweli huu siyo wa bahati mbaya ni wa kujitakia, ni wa makusudi ni wa kufumbia macho sheria zikivunjwa. 

Ni wa kubembeleza kura kwa njia ya ovyo kabisa ambayo haileti ustawi wa nchi hata kidogo.

Hakuna asiyekumbuka kwamba wakati Jiji la Dar es Salaam mwaka 1996 linavyunjwa na aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo, Frederick Sumaye, wamachinga walikuwa wametanda kila kona, walikuwa wamekuwa na ujasiri wa kujenga hata vibanda vya kuuza bidhaa ndogo ndogo na hata mitumba karibu kabisa na lango la Ikulu.

Eneo ambalo linajulikana kama eneo kuu la biashara la mjini kati (central business district – CBD) lilikuwa limejaa vibanda vya mbao vilivyojengwa ovyo ovyo. Kila upenyo ulizibwa, kisa uchuuzi; maeneo yote ya waenda kwa miguu yaligeuzwa kuwa sehemu ya kupanga bidhaa za wamachinga. Tume ilisafisha ghasia yote hii na kuacha jiji liking’aa.

Leo miaka 17 baadaye tumerudi kwenye tabu ile ile. Uchuuzi kila mahali; wamachinga wanatawala; barabara nzuri zilizojengwa na zinazoendelea kujengwa na kuwekwa sehemu ya waenda kwa miguu imegeuzwa uwanja wa bidhaa za wamachinga, uchuuzi huu inafanyika mchana na usiku, wenye mamlaka yao wapo na wanaona. 

Hawafanyi kitu. Kisa? Wanabembeleza kura!
Ziara ya Obama kwa mara nyingine tena imetukumbusha kwamba mjini mazingira yake yanapaswa kuwa masafi, shughuli zote mjini zinafanywa kwa mujibu wa sheria na kanuni za mipango miji. 

Ziara ya Obama walau kwa wiki moja imetukumbusha kwamba kumbe bado manispaa hizi zina askari mgambo wenye wajibu wa kusimamia sheria ndogondogo zilizotungwa pamoja na mambo mengine kuweka utaratibu wa kuendesha shughuli mjini.

Tunatamani sana kwamba baada ya Obama kuodoka jana na kwa baada ya Watanzania kumuonyesha ukaribu mkubwa kwamba ni watu wa amani na watulivu, sasa hali hii ya usafi itadumishwa.


Na Mhariri Nipashe

Polisi wakwama kumkamata mbaya wa Lema


Namba ya kituo iliyotumika katika mtandao wa simu kutuma ujumbe wa simu unaodaiwa kutoka kwenye namba za Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, kwenda kwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) ni ya Uingereza.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema jana kuwa ingawa uchunguzi unaendelea kumekuwa na ugumu wa kupata taarifa hizo kutoka kwa kampuni ya simu ya Uingereza zitakazoweza kupata ukweli wa mambo.
“Taratibu ndizo zinazoleta ugumu, lakini bado tunaendelea na uchuguzi,” alisema.

Mei 21, mwaka huu, Kamanda Sabas alimsafisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mulongo pale alipowaeleza waandishi wa habari kuwa uchunguzi wa awali kuhusu ujumbe unaodaiwa kutumwa na mkuu huyo wa mkoa umetumwa na mtandao wa simu ya nje.
Ingawa kwa wakati huo alikataa kutaja nchi lakini jana aliitaja Uingereza kuwa ndiko ujumbe huo ulikotumwa.

Katika kipindi cha mwishoni mwa Aprili mwaka huu, vyombo vingi vya habari vikiwamo radio, magazeti na mitandao ya kijamii viliandika na kutangaza habari iliyoelezea shutuma zilizotolewa na Mbunge Lema kuwa aliandikiwa ujumbe wa vitisho kwa njia ya simu na Mkuu wa Mkoa Mulongo ambao ulisomeka:

“Umeruka kihunzi cha kwanza nitakuonyesha mimi ni serikali, ulikojificha nitakupata na nitakupa kesi ninayoitaka mimi.”

Kwa mujibu wa Kamanda Sabas, ujumbe huo ulidaiwa kutumwa kutoka namba 0752960276 inayotumiwa na Mkuu wa Mkoa Mulongo kwenda kwenye namba 0764150747 inayotumiwa na Lema.

Alisema kufuatia tuhuma hizo, polisi walianza uchunguzi kwa kuzingatia kuwa Mulongo alikanusha kutuma ujumbe wa aina yo yote kwa Lema.

Obama: Uwazi wa Mikataba, Lumumba


Rais Barack Obama
Rais Barack Obama
Hatimaye Barack Obama, Rais wa Marekani anatembelea tena bara la Afrika. Hii itakuwa ni mara ya pili Obama kutembelea Bara hili alikotoka baba yake baada ya ziara yake ya kwanza mwaka 2009. Mwaka huo alitembelea Ghana na Misri ilhali mwaka huu anatembelea Senegali, Afrika Kusini na Tanzania. Ziara hiyo itakayoanza tarehe 26 mwezi Juni, itamfikisha Tanzania tarehe 1 Julai na kuondoka siku ya pili yake.
Uchaguzi wa Obama kuwa Rais wa Marekani ulipokolewa kwa shangwe Afrika nzima. Wakati Waziri wa mambo ya nje wa Nigeria alilia kwa furaha, nchi ya Kenya ilitangaza siku ya mapumziko na Rais wa zamani wa Afrika Kusini ndugu Nelson ‘Madiba’ Mandela alisema ‘ushindi wa Obama unawafanya Waafrika wathubutu kuota ndoto (Jarida la The Economist). Hapa Tanzania kulikuwa kuna shamra shamra za kila namna na magazeti yaliweka vichwa vya habari kana kwamba ni Rais wa Tanzania aliyechaguliwa. Waafrika walikuwa na matumaini makubwa sana na bwana Obama. Yamefikiwa?
Ni vema ifahamike kuwa Barack Obama ni Rais wa Marekani na siku zote atalinda maslahi ya Marekani tu. Kuwa na matumaini makubwa kwamba labda yeye angeliweza kuiweka Afrika mbele sana ilikuwa ni kujifurahisha tu nafsi. Maslahi ya Marekani ni ya kipaumbele kuliko kitu kingine chochote kwa Rais Obama. Kwa wengi Obama amekuwa kama amewavunja moyo.
Tanzania inapokea kiongozi wa Taifa kubwa duniani wa pili sasa ndani ya kipindi cha miezi 3 tu. Kwanza alikuja Rais wa China na sasa wiki hii anakuja Rais wa Marekani. Maneno ya mtaani na kwenye mabaraza ya majadiliano ni kwamba viongozi hawa wanakuja kugombea maliasili tulizo nazo kama gesi asilia na madini. Nadhani haya ni maneno ya kusema katika kupiga soga maana kunyonywa kwa rasilimali hakuhitaji Rais wa Marekani aje Tanzania. Makampuni yote makubwa yanayochimba dhahabu hapa nchini ni makampuni ya nje na marais wao hawakuja ili waweze kupata mikataba minono ya kuvuna utajiri wetu.  Katika kitalu namba 2 cha utafutaji wa mafuta na gesi huko Bahari Kuu kampuni ya kimarekani ya ExxonMobil ina ubia na kampuni ya Norway ya StatOil. Kampuni hiyo haikusubiri Rais wa Marekani aje ili wapate mikataba.
Kuna makampuni mengi sana ya kichina yanajenga barabara zetu hapa nchini yakiwa na mikataba minono sana. Kule Mchuchuma na Liganga kuna kampuni ya kichina inajiandaa na uchimbaji wa chuma na makaa ya mawe. Makampuni yote haya hayakusubiri Rais wao aje.
Hoja inayojengwa hapa ni kwamba ujio wa Marais mbalimbali nchini ni ujio wa kujijenga kidiplomasia na wakati mwingine kama sehemu ya kutuma ujumbe Fulani kwa dunia. Nchi inayotembelewa pia inaweza kuona kuwa diplomasia yake inaheshimiwa na mataifa yanayoitembelea.
Hata hivyo hii haiondoi ukweli kwamba Obama anakuja kwa ajili ya maslahi ya nchi yake kama ilivyo kwa wachina walivyokuja. Tumesikia Rais Obama ataambatana na mamia ya wafanyabishara kutoka Marekani kwa ajili ya kupata fursa za kuwekeza nchini. Pia tutasikia matangazo kuhusu msaada wa pili wa Millenium Challenge ambapo Wamarekani wanaendelea kumwaga pesa nchini kusaidia miundombinu lakini pia kushawishi kuungwa mkono na nchi zetu kwenye maamuzi Fulani Fulani jumuiya za kimataifa.
Tumesikia Obama atakwenda kutembelea mitambo ya kampuni ya Symbion. Hii ni mitambo ambayo miaka 4 iliyopita ilipigiwa kelele kuwa ni mitumba na hivyo TANESCO wasiinunue. Hawakununua na badala yake kampuni hiyo ya kimarekani ikainunua, wakaingia  mkataba na TANESCO kuwauzia umeme unaozalishwa na mitambo hiyo hiyo chakavu. Wakati tunasuburi kulipa takribani tshs 105 bilioni kwa Dowans baada ya kutubwaga kwenye kesi, tunasubiri kuona wanasiasa watakaokwenda kumsindikiza Obama kwenye matembezi hayo ya kutembelea mitambo chakavu.
Kampuni kubwa ya kutengeneza mitambo ya kuzalisha umeme ya GE imetangaza kuingia ubia na kampuni ya Symbion kuzalisha umeme nchini. Takribani 400MW zitazalishwa kutoka Mtwara na kuingizwa kwenye gridi ya Taifa. Pia sehemu kubwa ya umeme utakaozalishwa Mtwara tayari umepata soko kwenye kiwanda cha kuzalisha udongo ulaya (simenti) cha bwana Dangote kule Mtwara. Mtendaji Mkuu wa GE bwana Jeff Immelt ametangaza kuwa kampuni yake itauza mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi mingi zaidi Afrika Mashariki kuliko Marekani katika kipindi cha miaka mitatu ijayo. Ni biashara tu!
Nishati naona ni kipaumbele kikubwa sana kwa ziara ya Rais Obama. Kwa nchi kama yetu yenye watu asilimia 21 tu wenye umeme, ni dhahiri kipaumbele hiki watu wengi watakiiunga mkono. Hata hivyo Obama ni lazima asimame kidete kuhakikisha kuwa kampuni za nchini mwake zinazopata miakataba hapa nchini ziweke wazi mikataba hiyo na kulipa kodi inavyostahili. Makampuni ya mafuta kutoka Marekani hayana historia nzuri duniani na hivyo ni lazima tulisisitize mapema kabisa. Uwazi wa mikataba na uwezo wa kupambana na ukwepaji kodi ni muhimu sana katika vita dhidi ya Ufisadi na ubadhirifu.
Rais Obama atambue kuwa iwapo Tanzania ingekuwa inakusanya nusu ya kodi zinazokwepwa na makampuni makubwa yanayotumia mbinu kali, basi tungehitaji misaada ya Marekani na hapa nchini angekuja kama mbia wa kweli na sawa katika dunia. Hivyo ni vema aungane na Waziri Mkuu wa Uingereza kuhakikisha kuwa makampuni makubwa hayatumii ‘tax havens’ kukwepa kodi katika nchi kama Tanzania. Uwazi wa mapato yao na kilicholipwa kwa Serikali ni vema usisitizwe sana na Obama mwenyewe ili makampuni yao yasikie na yaache kupora utajiri wa Afrika kiujanja ujanja.
Patrice Lumumba
Mwisho ni vema kama Rais Obama ataomba radhi kwa ushiriki wa Marekani kwenye mauaji wa Waziri Mkuu wa kwanza wa Kongo Patrice Lumumba. Hivi Tanzania inahangaika zaidi ya uwezo wake kupeleka majeshi huko mashariki ya Kongo kulinda amani. Waafrika wengi tunaamini kuwa mauaji ya Lumumba ilikuwa ni kama laana kwa Taifa lile na hivyo limekuwa ni taifa la vurugu na vita licha ya utajiri mkubwa ulioko nchini humo. Nyaraka za CIA zinaonyesha dhahiri kuwa Rais wa Marekani wa wakati huo Lyndon Johnson aliagiza kuuwawa kwa mwanamapinduzi Patrice Lumumba. Kuwaomba radhi Waafrika na hasa Wakongo kuhusu mauaji ya Lumumba ni jambo litakaloweza kusaidia sana kurejesha amani Kongo.
Karibu Afrika, Karibu Tanzania ndugu Barack Hussein Obama.
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. harod tz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger