Tofauti ya ubongo wa
mwanamke na wa mwanaume. (Human brain analysis) - By Giningi Siyabonga
(Braza Joni)
1. Ubongo wa mwanamke unaweza kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja;
mfano kuzungumza kwenye simu na kufuatilia kipindi kwenye TV. Mwanaume
hawezi.
2. Lugha: wanawake wanaweza kujifunza lugha nyingi kwa urahisi. Chukua
mtoto wa kike na wa kiume wenye umri wa miaka mitatu. Mara nyingi wa
kike atakuwa anajua maneno mengi kuliko wa kiume.
3. Kusema uongo: mwanaume akimdanganya mwanaume uso kwa uso ni rahisi
kushtukiwa. Wanawake hugundua ukweli kupitia uso wako kwa 70%, kupitia
body language yako 20% na 10% kupitia maneno yako. Ubongo wa mwanaume
hauna uwezo wao ndiyo maana ni rahisi mwanamke kumdanganya mwanaume uso
kwa uso. Guys, next time ukiwa unamdanganya msichana ni better mkiwa
hamko uso kwa uso.
4. Uwezo wa kutatua matatizo: mwanaume akiwa na matatizo, ubongo wake
huyachukua na kuyatenga katika makundi mbalimbali na kisha huanza
kutafuta suluhisho moja baada ya jingine. Mwanamke akiwa na matatizo
ubongo wake hauwezi kuyatenga na badala yake hutaka mtu amsikilize.
Baada ya kumwambia mtu matatizo yake yote akili yake hupata kiwango
fulani cha utulivu na huwa mara nyingi hajali kama yatatuliwa au la.
5. Mahitaji: Wanaume wanahitaji heshima kwenye jamii, mafanikio, sifa,
nk.; wanawake wanapenda mahusiano, familia, marafiki, etc.
6. Kuongea: mwanamke mara nyingi hutumia lugha ya kificho. Mwanaume
hutumia lugha ya moja kwa moja. CHANZO NI MASANJA MKANDAMIZAJI
Post a Comment