.
kuna vitu ambavyo mwanamke hutakiwi kukosa katika nyumba yako
nitaviongelea kwa mafumbo ili kujuwa undani zaidi basi wewe mwanamke
usikose mafundo hayo jumapili ijayo 7/7/2013 na kila kitu kati ya
nitakavyoandika hapa leo vitakuwepo siku hiyo.
Kwanza kabisa mwanake nyumbani kwako nilazima uwe na osheo la sufuria
inahusu nini mwanamke ukasonga ugali na kushindwa kuosha sufuria
ikabaki na ukoko, ni lazima uwe na kosheo tena sio kosheo tu linalomudu
usafi bibi....
Pili mwanamke kwenye nyumba yako chupa ya chai muhimu, familia na
wageni wako asubuhi au jioni lazima wanywe chai ya moto yenye ujotojoto
haipendezi wala haina ladha mwanamke ukawatengea wageni chai iliyopoa.
Tatu mwanamke lazima uwe na fridge ya kuwekea maji jamani dar hii
joto jingi mtu unataka ukirudi nyumbani wakati wote maji ya wepo unywe
ukate kiu, na kiu ya dar kwa maji ya moto wala haikatiki ila kwa wale
ambao hawawezi kunywa maji ya baridi basi hata ya moto pia ni sawa.
Nnne mwanamke lazima ndani kwako uwe na kabati tena zuri kwa ajili ya
kuwekea nguo na lengine vyombo ili nyumba yako ipangike sio wageni
tunakuja unakuta patupu mwanamke au kila kitu vuruguvurugu hujui hiki
kipo wapi kile kimeenda wapi shoga yangu utaaibika.
Nimeonglea kikungwi zaidi na najuwa wengi sana watakuwa hawajaelewa
ila kwakuwa utakuja kufundwa naamini utaelewa yote hayo, nimeandika
hivyo kukata ukali wa maneno maana ni makubwa na mazito hayastahili
kuandikwa hapa.
Post a Comment