ngekuwa wewe Ungefanyaje ?? Balaa Hili
Mdada mmoja mke wa mtu alikuwa akisumbuliwa sana na jamaa mmoja
aliyekuwa akimtaka kila siku, hatimae akamwambia mumewe. Mume akamwambia
mkewe, we kubali tuu, ila mwambie aje mlale hapa kwetu, mi ntajificha
uvunguni na panga. Akisha ingia ukiona kamaliza kuvua nguo we ning’iniza
mkono anza kuuchezesha, mi nikiuona ntatoka uvunguni na kumfunza adabu.
Mdada akafuata masharti ya mumewe na hatimae wakaingia chumbani na yule
bwana , mumewe akiwa tayari na panga uvunguni mwa kitanda. Jamaa
alipovua shati, mke alishangaa kuona ana makovu makubwa kifuani na
mgongoni;
MKE: Heee mbona una makovu hivyo??
JAMAA: Niwe mkweli tuu, kwako dia!! mie nina tatizo sana la kupenda wake
za watu, waume wengi wamekuwa wakipanga kunifumania, nilishafumaniwa
mara kumi na tisa, na wote walionifumania niliwaua. Ila jaribio la
mwisho nilidakwa na mapolisi nikatumikia kifungo cha miaka 27 jela,
Lakini ninavyopenda wake za watu sitaacha kuua. Hivi sina muda tangu
nitoke huko jela hivyo nina ukame wa punda na nilipokuona moyo wangu
ukakudondokea. Na nitatulia na wewe.
MKE: Heee! Haiwezekani jamani!!….jamaa akaendelea kuvua nguo alipomaliza
mdada akaanza kujitahidi kuning’iniza mkono ili mumewe atoke uvunguni
aje kumuokoa, mume akabana kimya, kila mdada akijitihadi kupunga mkono
hakupata jibu, mdada akalalamika mpaka jamaa akamaliza shughuli zake
akatokomea.
MKE: Huku akilia, ndio nini umenifanyia? Mbona hukutoka??
MUME: We we we, Weeeee mama naniii!!.. mwenyewe umesikia keshaua 19
ulitaka niwe wa ishirini?
Post a Comment