Latest Post

Diamond

Written By Unknown on Monday, July 15, 2013 | 01:58

MAPENZI NI HISIA TAMU ZENYE CHUNGU, USICHEZEE!-2

Written By Unknown on Saturday, July 6, 2013 | 01:48


KUNA mambo mengi sana katika maisha yanayokosesha furaha lakini kwa utafiti wa harakaharaka, mapenzi ndiyo yanaongoza kwa kuwanyima watu raha.
Hii inamaana kwamba, si kila aliye kwenye mapenzi hana furaha, bali ikitokea furaha iliyopo kwenye mapenzi ikapotea, mhusika huumia mara mia zaidi ya akipata hasara katika biashara zake!
Ndugu zangu huu ndiyo ukweli ulivyo. Familia ikiwa yenye migogoro, maendeleo yatakuwa ni ndoto. Ndiyo maana tunajifunza mapenzi kila kukicha.
Katika matoleo yaliyopita, nilianza kwa kueleza kuhusu wale ambao wanarukia mapenzi bila kuwa na uhakika na hisia zao, mwishowe wanaumia au wanaumizwa!
Mwenzako anawekeza kwako akiamini yupo na mtu sahihi, kumbe kichwani mwako unamfanya daraja. Sawa, acha awe daraja na akuvushe salama, vipi moyoni mwake? Unajua anawaza nini?
Unajua mwisho wa fikra zake katika maumivu ya mapenzi? Unajua maamuzi ambayo anaweza kuyachukua? Kwa hakika kila kitu ni giza maana huwezi kuingia ndani ya moyo wa mwenzako na kujua kile anachowaza.
Tuendelee kujifunza.

ACHA MAPENZI YA KUIGIZA
Wapo wanaoingia kwenye uhusiano hata kama hawana lengo la kuwachuna wenzao lakini hawana uhakika na hisia zao. Wanaamua kujaribu kuona kama labda baadaye wanaweza kupenda.
Kutokana na hilo basi, kinachofuata inakuwa ni kufanya maigizo tu na si kweli kwamba wapo kwenye uhusiano ‘seriously’. Hili ni tatizo.
Wapo wenzangu na miye wanaojiita marioo, wanajiingiza hata kwa majimama ili wapate fedha, siyo sawa. Hutaona athari zake haraka, lakini ukweli ni kwamba unajiweka katika nafasi ya kupoteza hisia za kupenda hapo baadaye.

NI HISIA TAMU ZENYE CHUNGU
Utamu wa mapenzi unakuja pale wawili wanapokutana wakiwa na hisia sawa. Uchungu hutokea pale ambapo mmoja anajua kwamba yupo kwenye uhusiano ulio sahihi wakati mwingine akiwa na uhakika kuwa anazuga tu kwa muda,
Kumbuka hapo tayari kunakuwa na hisia mbili tofauti zinazosafiri pamoja. Moja inakuza upendo, nyingine inakuza chuki. Unajua mwisho wake? Ni kama nilivyoeleza kwenye kipengele kilichopita.

KUTOKA KWANGU
Ya nini yote hayo? Hebu simama kwa miguu yako miwili. Acha kucheza na hisia za mwingine. Heshimu moyo wa mwenzako kama unavyoubembeleza wako.
Acha kumpotezea muda mwenzako. Usiingie kwenye uhusiano kwa sababu ya kitu maana ipo siku inaweza kukutokea puani.
Kama wewe huna nia ya kupenda au kupendwa, waache wenzako wenye lengo hilo, wewe uendelee na mambo yako huko chochoroni, tena uwe wazi, kuwa upo kazini!

Katika Nyumba yako Mwanamke........


.

kuna vitu ambavyo mwanamke hutakiwi kukosa katika nyumba yako nitaviongelea kwa mafumbo ili kujuwa undani zaidi basi wewe mwanamke usikose mafundo hayo jumapili ijayo 7/7/2013 na kila kitu kati ya nitakavyoandika hapa leo vitakuwepo siku hiyo.

Kwanza kabisa mwanake nyumbani kwako nilazima uwe na osheo la sufuria inahusu nini mwanamke ukasonga ugali na kushindwa kuosha sufuria ikabaki na ukoko, ni lazima uwe na kosheo tena sio kosheo tu linalomudu usafi bibi....

Pili mwanamke kwenye nyumba yako chupa ya chai muhimu, familia na wageni wako asubuhi au jioni lazima wanywe chai ya moto yenye ujotojoto haipendezi wala haina ladha mwanamke ukawatengea wageni chai iliyopoa.

Tatu mwanamke lazima uwe na fridge ya kuwekea maji jamani dar hii joto jingi mtu unataka ukirudi nyumbani wakati wote maji ya wepo unywe ukate kiu, na kiu ya dar kwa maji ya moto wala haikatiki ila kwa wale ambao hawawezi kunywa maji ya baridi basi hata ya moto pia ni sawa.

Nnne mwanamke lazima ndani kwako uwe na kabati tena zuri kwa ajili ya kuwekea nguo na lengine vyombo ili nyumba yako ipangike sio wageni tunakuja unakuta patupu mwanamke au kila kitu vuruguvurugu hujui hiki kipo wapi kile kimeenda wapi shoga yangu utaaibika.

Nimeonglea kikungwi zaidi na najuwa wengi sana watakuwa hawajaelewa ila kwakuwa utakuja kufundwa naamini utaelewa yote hayo, nimeandika hivyo kukata ukali wa maneno maana ni makubwa na mazito hayastahili kuandikwa hapa.

Kutongonolewa vema

angry woma



Kutongonolewa vema
Kunakusababishai mood mbaya ewe mwanamke!

Sote tunatambua kuwa ngono ni muhimu ktk maisha yetu hasa wanawake, mwanamke anaefanya ngono angalau mara mbili kwa wiki "immune hu-function vema kabisa.

Mwanamke anaepata mizunguuko mingi huwa na furaha na kujihisi anavutia kuliko yule ambae anafanya mara moja kila baada ya wiki mbili kama sio mara moja kwa mwezi.

Vilevile mwanamke asiepata ngono vizuri....hafanyi vema kutokana na sababu tofauti husumbuliwa na chuki/hasira bila sababu ya msingi na pia huichukia ngono hali inayomfanya aendelee kutokufurahia kwa vile ana negative thought kuhusiana na tendo zima.

TUZUNGUMZE MAPENZI!

Kila mtu anajua habari za mapenzi,hata wewe unayesoma habari hii unajua habari hizi. Mapenzi ni matunda matamu na pia ni matunda machungu.Sijui inategemea nini lakini nadhani ni kadri unavyoyapata,unavyoyala,na unavyojisikia wakati unaanza kula au unapomaliza.
Blog hii ni ya watu wazima,watu wanaojua nini maana ya mapenzi au wanaojaribu kujua zaidi.Nimeamua kuanzisha blogu hii kwa sababu najua ipo haja ya watu kuendelea kubadilishana mawazo juu ya mapenzi,ngono na mengineyo yanayohusiana na miili yetu,zikiwemo afya zetu.Si mnajua kwamba kitumbua siku hizi kimeingia mchanga ndugu zangu?

Kwa hiyo keti kitako tuanze kuyachambua masuala ya mapenzi. Kwa utaalamu wangu wa masuala haya nadhani nitakuwa tayari kujibu maswali yenu,hoja zenu nk kuhusiana na mapenzi,kujamiiana(ngono) na mengi mengineyo. Jisikie huru kunitumia email au kuuliza swali lako hapa hapa,nitakujibu. Lakini kwa kuanzisha hoja,hebu niambie,mapenzi ni nini kwa jinsi unavyoelewa wewe?Ni kwanini eti watu wanauana,wanafarakana,wanachinjana,nchi zinaingia kwenye vita kisa mapenzi? Je hayo yanabakia kuwa mapenzi au chuki? Kuna uhusiano gani kati ya mapenzi na wivu?Yupi ana nguvu kumshinda mwenzake?

WANAWAKE NA PESA


Msomaji mmoja wa blog hii kuhusu mapenzi (hakupenda kuweka jina lake) amekuwa wa kwanza kuuliza swali.Nitaliweka swali lake kwa kutumia italics likifuatiwa na jibu langu. Nitakuwa najaribu kuyaweka majibu yangu kwa ufupi sana(not in details) ili kuokoa nafasi na pia muda wako. Hata hivyo,tunaweza kuwasiliana kwa email kama utahitaji details zaidi na pia michango,mawazo,maoni nk yanakaribishwa sehemu ya mbele ya maoni.

SWALI:Sasa mimi nauliza kwa nini wasichana wengi wanapenda wanaume wenye pesa hata kama wana uwezo wa kupata pesa pia.Kwa nini wasijiamini nao kama wanaume na kufikiria kuwa pesa siyo jambo la maana sana kama unampenda mwenzio?

JIBU:Swali hili lina historia ndefu sana na ya aina yake. Ni swali lenye umri mkubwa pengine kama ilivyo dunia yetu. Ni swali zuri sana. Mara nyingi limeulizwa kwamba hivi mwanamke anataka nini zaidi,pesa,ulinzi au mapenzi na mapenzi motomoto kitandani?(Wenzetu wazungu lugha yao inaweza kutenganisha dhana hizi mbili kirahisi zaidi;love or good sex) Kwa bahati mbaya hata wanawake wenyewe wamejikuta kila mara wakipambanua mambo yote haya kwa sababu kwanza wanaume wenye sifa zote hizo hapo juu kwa pamoja ni kama hawapo na dunia imebadilika na inaendelea kubadilika.

Kabla sijaendelea mbele naomba ieleweke kwamba sio kila mwanamke anaweka pesa mbele na sio kila mwanamke duniani bado anaamini kwamb a yeye ni mtu wa kupokea,kuhudumiwa na kutunzwa tu.. Hali ni tofauti baina ya sehemu na sehemu,nchi na nchi,bara na bara,tamaduni na tamaduni. Kwa mfano hapa ninapoishi tamaa ya wanawake kupenda na kuthamini pesa inazidi kupungua kadri siku zinavyokwenda. Siku hizi wanawake nao wapo mstari wa mbele kuchangia kwa njia zote zinazowezekana kuboresha maisha na kwa maana hii mapenzi.

Sifa zinaenda kwa wale wanawake wanaojulikana kama “feminists” ambao kwa namna moja au nyingine wanachojaribu kufanya ni kumkomboa mwanamke kutoka kwenye fikra za yeye kuwa chombo cha kupokea tu bila kushiriki kwenye kutafuta na kutoa.

Pamoja na juhudi za dhati za wanasaikolojia katika kubadili muelekeo wa fikra za wale wanawake wanaothamini pesa na kubakia wakidhani kwamba jukumu la kutoa pesa,kuchangia matumizi,kuthamini mapenzi zaidi haliwahusu,bado wapo wengi wenye msimamo tofauti.Wao bado wamegubikwa na utando wa historia,utando wa saikolojia na pia utando wa nafasi ya mwanaume dhidi ya mwanamke au dhidi ya jamii inayomzunguka.

Msimamo wao ndio muuliza swali wetu, anaouwekea msisitizo;kwamba kwanini hata wale walio na hali nzuri kifedha bado wanadhani sio jukumu lao kusaidia,kuchangia katika matumizi?

Sababu kubwa,kama nilivyoanza kuanisha hapo juu ni fikra. Kihistoria,tangu mwanzo wa dunia hii mwanaume amekuwa mtafutaji na mwanamke akabakia nyumbani kulea watoto,kutunza kaya na kuhakikisha kwamba familia inakuwa bora. Katika nchi zetu za kiafrika,kwa mfano,utaratibu ukawa binti akue,akishavunja ungo basi aoelewe akaanzishe familia yake.Wazo la yeye kuandaliwa kama mtafutaji halikuwepo kabisa. Kwa bahati mbaya dunia tunayoishi hivi leo inatoa nafasi kidogo sana kwa ustawi wa taratibu kama hizo.Lakini je,fikra au utaratibu huo umetokomea vichwani mwa watu,hususani wanawake wenyewe? Jibu rahisi ni kwamba bado fikra ile ya mapokeo ipo miongoni mwa wanawake wengi.

Sababu ya pili ni ya asili kimaumbile na kisaikolojia vile vile. Kimaumbile mwanaume ameumbwa awe mkakamavu zaidi,awe mlinzi wa mwanamke.Ingawa siku hizi mambo yanazidi kubadilika ambapo utaona wanawake wengi katika shughuli ambazo hapo zamani zilidhaniwa kuwa za wanaume peke yao,bado kwa kiwango kikubwa, hali imebakia kama ilivyokuwa enzi za Adam na Hawa. Sasa “protection” hii haishii kwenye ulinzi wa kimaumbile tu kwamba nyumba ikivamiwa mwanaume ndiye anategemewa zaidi kuongoza mapambano dhidi ya wavamizi,bali huenda pia hata kwenye financial protectionism ambapo bila kujali mwanaume ana kiasi gani cha fedha,bado anategemewa kuwa mtoaji.

Mwishoni nashauri pia tusisahau watu wanaoitwa “sugar mummies”. Hawa pia ni wanawake ambao msimamo wao ni tofauti kabisa na wanawake wengi ingawa motives zao ni tofauti na mara nyingi zinaeleweka.Pengine siku moja tutapata nafasi ya kuzungumzia saikolojia zao pia.

KIDOKEZO: Hivi unafahamu kwamba mfalme wa Morocco wa karne ya 16 (Moulay Ismail) alikuwa na watoto wanaokadiria kufikia 1,042?

PICHA KALI ZA MATUKIO YANAYOJIRI KWENYE MITAA MBALIMBALI !








 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. harod tz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger