Baada ya kufunguliwa shtaka hilo, Lissu ambaye alikuwa wakili wa Sugu aliitaka mahakama ifutilie mbali shtaka hilo kwani halina msingi wowote wa kisheria na baada ya mabishano ya kisheria baina ya Lissu na wanasheria wa serikali kushindwa kuthibitisha kuwa neno -------- ni lugha ya matusi, hakimu ameamua kufuta shtaka hilo na ametangaza kuwa Sugu yuko huru na hana kesi ya kujibu.

Muda huu ndio wanaondoka mahakamani, Sugu, Lissu na baadhi ya wabunge na viongozi wa CHADEMA ambao walikuwa mahakamani hapo.

My take:
Polisi na serikali, mnaendelea kujidhalilisha kwa kufungua kesi ambazo zinaendelea kuwavunjia heshima mbele ya mahkaama na umma wa watz. Acheni kufuata maelekezo ya kina Mwigulu, hawajui sheria, hawajui misingi ya kufungua kesi, nyie kila siku mtakuwa mnafungua kesi mpaka lini wakati mnashindwa.