Home » » HII INAKUHUSU SANA...!!

HII INAKUHUSU SANA...!!

Written By Unknown on Saturday, July 6, 2013 | 00:41


Asubuhi ya leo nilikuwa na  press conference ya Tamasha la matumaini
iliyofanyika kwenye hotel ya
Atriums maeneo ya kijitonyama, Binafsi mimi na wasanii
 wengine wa Bongo Flavour,Bongo Movie,wabunge,
pamoja na wanamasumbwi watakaoshiriki walikuwepo pia kwenye
mkutano huo na waandishi wa habari....!!
Nia ni kuzungumzia mchango wetu na wa kila mmoja kwenye
Tamasha la Matumaini litakalofanyika
tarehe 7.7.2013 kwenye uwanja wa Taifa....
Madhumuni ya Tamasha ili ni kama jina linavyojieleza, madhumuni ya
 kwanza ya tamasha ili ni kurejesha
matumaini miongoni mwa watanzania ambapo kauli mbiu ya mwaka
huu inasema ; 'Licha ya tofauti zetu za kidini
na kiitikadi,lakini sisi sote ni Watanzania....!!Aidha
 madhumuni ya pili ya tamasha hili ni kuchangia mfuko wa elimu wa Tanzania,ambayo tangu mwaka jana 
imekuwa katika kampeni ya kukusanya fedha kwaajili
ya ujenzi wa mabweni ya wasichana katika shule za sekondari
nchini..Sehemu ya faida itakayopatikana katika tamasha ili zitawezesha
mfuko huo wa elimu ya juu...
Burudani mbalimabli zitakuwepo siku hiyo ni kuanzia muziki wa dansi,
muziki wa taarabu,muziki wa injili,muziki wa kizazi kipya,
soka na ndondi....!!
Upande wa soka kutakuwa na mechi kati ya wabunge wa Bunge
la jamuhuri ya muungano wa Tanzania
baina ya wabunge wa simba na yanga...!
Katika ndondi atakuwepo msanii wa Bongo movie Jacquline
wolper atazichapa na Mbunge wa chadema
Halima Mdee uku Mbunge wa Chadema kwa wanaume
akizichapa na Msanii wa bongo movie
vicent kigosi maarufu kama Ray...!!
Katika kupendezesha usiku wa matumaini kutakuwa
Pambano la kimuziki wa Kimataifa
kati ya kenya na Tanzania,kutoka Tanzania tutawakilishwa
 na Rais wa wasafi  Diamond Platnumz
na kutoka Kenya watawakilishwa na Prezzo,
katika mpambano wa Ngumi
za Kimataifa kati ya Kenya na watanzania kati ya Thomas
Masharia wa Tanzania atazipiga na
Bondia Patrick amote kutoka kenya na Thomas Miyeyusho
atapanda ulingoni na Shadrack
Muchanje kutoka kenya mabondia hawa watagombea ngao ya
 Amani ya Afrika Mashariki...!!
Siku hiyo viingilio vitakuwa 5,000/= ndio kiingilio cha chini kuliko
vyote viti vya mzunguruko wa juu na wakati Tsh 10,000/=
utakuwa vitii vya orange na bluu na V.I.P iatakuwa kwa Tsh 20,000/=
Tamasha litaanza kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 6 usiku

Zifuatazo ni Picha na waandishi tofauti wa Habari...!!
Nilipowasili hoteli ya Atriums nilikuta tayari wasanii
wakongwe wa Bongo movie wakiwa
wameshawasilii wakisubiri mkutano na waandishi wa habari...


Muongozaji wa Tamasha la Matumaini akizungumza na waandishi wa habari ...!!

Big Boss Jay B kigogo mtu mbaya along side Jacquline wolper......!!

Jacquline wolper akizungumza jambo...!!

Ray kigosi akizungumza juu ya mpambano wake na
Mbunge wa Chadema Mhe.Zitto kabwe






Muda ulipowadia mimi kuzungumza juu ya mpambano wangu wa kimataifa
na msanii toka kenya ''watanzania wawe na Imani na mimi na ushindi utabakia kwetu
hapa hapa nimejianda vya kutosha mimi na crew yangu nzima ya wasafi...''

Qboy Msafii wa akiwa na Jay B..!!

Baada ya shughuli nzima kukamilika ilikuwa ni safari ya mimi
 kuhamsha na kuelekea kwenye
michakato mingine ya kimaisha....!!
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. harod tz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger