Leo jioni wakati natoka katika shughuli zangu nilipita maeneo ya Mwenge
pale stand ya mabasi nimekuta kweupe wale vijana wanao uza nguo kwa
kupanga chini na kuzishika sikuwaona ...nikauliza nikaambiwa wamefukuzwa
kwa ajili Oboma Anakuja...Mmhhh Kazi kweli kweli ...
Wakati bado nashangaa shangaa Mara likaja gari la Polisi na Wale mgambo
wa jiji...Mara nikaona watu wanakimbia huku na kule ...Kushangaa kumbe
wale wamachinga bado wapo ila wanauza kwa kujificha ficha kwenye
vichochoro vya maduka..Sasa Kimbembe kikaanza wale wanamgambo
wakawafuata huko huko na kuanza kuwapiga na kuwavunjia meza na viti
vyao...Kwa kweli iliniuma sana kuona watanzania wenzetu wakifanyiwa
hivyo ....Bado sijapata jibu ...siko zote mbona hawakufukuzwa ?? Huu
Ugeni ndio imekuwa Nogwaaaaa....
Na uhakika kuna ambao wanalisha na kutunza familia kwa kazi hizi za
umachinga sasa watakula wapi kama hali ndio hiyo????
Original from:
Post a Comment