Mchezaji
wa bora wa mashindano ya kombe la mabara Neymar ana miaka 21 tu ,
lakini ni mmoja ya wachezaji wa Amerika ya Kusini ambao wanaweza
kuwafanya watu wazimie kwa kujawa na furaha kwa kumuangalia tu mchezaji
huyo wa kibrazili na huku akiwa anakaribia kujiunga rasmi na Barcelona,
umaarufu wake unaweza ukazidi kukua mpaka kwenye mabara mengine.
Katika
kuonyesha ni namna gani anakubalika huko barani Amerika, watu nchini
Bolivia wamewapa watoto wao jina la Neymar katika hali ya kumtukuza
winga huyo wa kibrazili.
Kutoka Sambafoot:
"Tunaamini miaka 17 ijayo vijana wengi wa wakati huo watakuwa na jina la Neymar kwa sababu ya huu mtindo mpya ulioingia,' alisema msajili wa raia Remigio Condori .Kwa mujibu wa gazeti la Bolivia La Razon, watoto wawili kati y 10 wanaozaliwa kwenye nchi hiyo wamekuwa wakipewa jina la mchezaji huyo wa selecao. Na wanatabiri kwamba suala hili litazidi kukua kwa kuwa hata baadhi ya wanaume hasa kwenye mji wa La Paz wamekuwa wakijipa jina la nyota huyo wa Barcelona
Post a Comment