Home »
BURUDANI
,
MAGAZETI
» PICHA YA SIKU: BARCELONA WAMUONDOA THIAGO ALCANTARA KWENYE TANGAZO LA JEZI NA TOUR KWENYE AKAUNTI YAO YA INSTAGRAM
PICHA YA SIKU: BARCELONA WAMUONDOA THIAGO ALCANTARA KWENYE TANGAZO LA JEZI NA TOUR KWENYE AKAUNTI YAO YA INSTAGRAM
|
Klabu
ya Barcelona imemkata mchezaji wao Thiago Alcantara anayewania na
Manchester United kwenye tangazo la kuitangaza tour yao pamoja na jezi
mpya waliloweka kwenye akaunti yao rasmi ya mtandao wa kijamii wa
Instagram. Thiago kwa muda mrefu sasa ametajwa kutaka kuondoka kwenye
klabu hiyo huku vyombo vya habari vikiripoti kwamba ndani ya wiki hii
mchezaji huyo atakuwa ameshajiunga na United chini ya David Moyes. FC
Barcelona na United zote hazijakanusha wala kukubali taarifa hizi - ila
kwa kitendo cha Barca kukata sura ya Thiago kwenye picha ambayo mwanzoni
alikuwepo kimezidi kuzipa nguvu tetesi za mchezaji kuhamia Man United.
Lakini hizi zote ni tetesi na hakuna kilichothibitishwa. |
|
Picha
ya juu inaonyesha ilivyokuwa mwanzo Thiago akiwepo - wakati hii ya
chini ni ya leo ikiwa sura ya Thiago Alcantara haijakwatwa. |
Post a Comment