Zdravko
Mamic ni ni mkurugenzi wa michezo wa Dinamo. Amekuwa maarufu sana kwa
tabia yake ya kuwatolea maneno machafu baadhi ya waandishi wa habari,
akiwatishia kuwafanyia vurugu na kuwatukana wao na kazi yao. Pia amekuwa
akihusishwa sana na sajili tata za wachezaji hasa wa nchi hiyo. Aliwahi
kukamatwa baada ya kumtukana waziri wa michezo wa Croatia, lakini
pamoja na vituko kocha huyu ana mazuri yake. Ni genius linapokuja suala
la kufanya biashara ya wachezaji.
Katika
kipindi cha miaka 10, tangu Zdravko Mamic ajiunge na Dinamo Zagreb,
klabu hiyo imejipatia kiasi cha 160 million kutokana na mauzo ya
wachezaji.
Dinamo
Zagreb sio timu inayofanya biashara ya kuuza sana wachezaji barani ulaya
kama ilivyo kwa Porto, lakini hawapo mbali kwenye. Benfica na Udinese
pia nao wanafuatia, lakini inabidi vilabu hivi vyote vina misuli ya
kifedha kuliko klabu hii ya Croatia.
Luka Modric mmoja ya wachezaji wanamuingizia fedha nyingi Mamic |
Mamic
anapata fedha nyingi kwa kukubali kuwauza wachezaji kwenda kwenye vilabu
vikubwa. Mfano mzuri ni dili aliloingia na Luka Modric - walikubaliana
na mchezaji huyo kupata asilimia 20 ya mshahara wake atakaokuwa akilipwa
na klabu yake. Pia dili hilo limeendelea mpaka sasa mchezaji huyo akiwa
na Real Madrid - kwa makataba wa miaka mitano na Madrid - Luka Modric
atampatia kiasi kisichopungua 900 000 Euros Zdravko Mamic.
Tangu awe mkurugenzi wa ufundi wa Dinamo mwaka 2003, ameshawabadilisha makocha 15 tofauti - waliokuwa wanatofautiana nae kwenye suala la kuuza wachezaji pale anapoona kuna maslahi yake yake binafsi.
BAADHI YA UHAMISHO WALIOWAHI KUFANYA DINAMO ZEGREB
Luka Modric to Tottenham , €21 million
Mateo Kovacic to Inter Milan , €15 million
Eduardo da Silva to Arsenal, , €15 million
Vedran Corluka to Manchester City, , €13 million
Dejan Lovren to Lion , €9.5 million
Mario Mandzukic to Wolfsburg, , €9 million
Pia hivi sasa Mamic yupo katika mazungumzo na Tottenham katika kukamilisha baishara ya kuwauza wachezaji wawili Tin Jedvaj na Alen Halilovic ambaye anatajwa kuwa mrithi wa Luka Modric. Dili hilo linatajwa kuwa na thamani ya zaidi ya paundi millioni 18 - na hapo Mamic ana kato lake pamoja na kuwa na mikataba binafsi na wachezaji hao wawili.
Taarifa nchini Croatia zinasema Mamic yupo katika matayarisho ya kuanzisha kampuni ya uwakala wa wachezaji, ili kufuata nyayo za wakala maarufu barani ulaya Jorge Mendes.
Taarifa nchini Croatia zinasema Mamic yupo katika matayarisho ya kuanzisha kampuni ya uwakala wa wachezaji, ili kufuata nyayo za wakala maarufu barani ulaya Jorge Mendes.
Post a Comment